Psalms 25

Kumwomba Mungu Uongozi Na Ulinzi

Zaburi ya Daudi.

1 aKwako wewe, Ee Bwana,
nainua nafsi yangu,
2 bni wewe ninayekutumainia,
Ee Mungu wangu.
Usiniache niaibike,
wala usiache adui zangu wakanishinda.
3 cKamwe hakuna hata mmoja anayekutegemea
atakayeaibishwa,
bali wataaibishwa
wafanyao hila bila sababu.

4 dNionyeshe njia zako, Ee Bwana,
nifundishe mapito yako,
5 eniongoze katika kweli yako na kunifundisha,
kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu,
nalo tumaini langu liko kwako wakati wote.
6 fKumbuka, Ee Bwana, rehema zako kuu na upendo,
kwa maana zimekuwepo tangu zamani.
7 gUsizikumbuke dhambi za ujana wangu
wala njia zangu za uasi,
sawasawa na upendo wako unikumbuke,
kwa maana wewe ni mwema, Ee Bwana.

8 h Bwana ni mwema na mwenye adili,
kwa hiyo huwafundisha wenye dhambi njia zake.
9 iHuwaongoza wanyenyekevu katika haki,
naye huwafundisha njia yake.
10 jNjia zote za Bwana ni za upendo na uaminifu
kwa wale wanaoshika shuhuda za agano lake.
11 kEe Bwana, kwa ajili ya jina lako,
unisamehe uovu wangu, ijapokuwa ni mwingi.
12 lNi nani basi, mtu yule anayemcha Bwana?
Atamfundisha katika njia
atakayoichagua kwa ajili yake.
13 mMtu huyo atafanikiwa maishani mwake,
nao wazao wake watairithi nchi.
14 nSiri ya Bwana iko kwa wale wamchao,
yeye huwajulisha agano lake.
15 oMacho yangu humwelekea Bwana daima,
kwa kuwa yeye peke yake ndiye ataitoa
miguu yangu kutoka mtego.

16 pNigeukie na unihurumie,
kwa maana mimi ni mpweke na mwenye kuteseka.
17 qShida za moyo wangu zimeongezeka,
niokoe katika dhiki yangu.
18 rUangalie mateso na shida zangu
na uniondolee dhambi zangu zote.
19 sTazama adui zangu walivyo wengi,
pia uone jinsi wanavyonichukia vikali!
20 tUyalinde maisha yangu na uniokoe,
usiniache niaibike,
kwa maana nimekukimbilia wewe.
21 uUadilifu na uaminifu vinilinde,
kwa sababu tumaini langu ni kwako.

22 vEe Mungu, wakomboe Israeli,
katika shida zao zote!
Copyright information for SwhNEN